26.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Bosi BMT ahofia kutumbuliwa

Mohamed Kiganja
Mohamed Kiganja

Na WINFRIDA NGONYANI-DAR ES SALAAM

KAIMU Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo nchini (BMT), Mohamed Kiganja, amesema hawezi kufanya kazi na wadau wa michezo wasiolipa kodi.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya katibu huyo kutoa agizo kwa vyama na mashirikisho yote ya ngumi nchini, kuhakikisha wanapata kibali kutoka kwa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC).

Hatua hiyo ya Serikali inapingwa vikali na vyama mbalimbali vya ngumi vinavyodai kigogo huyo wa Serikali kukiuka kanuni na sheria za Baraza hilo.

Akizungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalumu, Kiganja alisema vyama hivyo vinatakiwa kutekeleza agizo hilo ili viweze kufanya kazi kwa taratibu na sheria za nchi ikiwamo kulipa kodi.

“Agizo hili linapaswa kutekelezwa na vyama vyote, hakuna sheria yoyote iliyokiukwa, sisi kama Baraza tunaitambua TPBC kuwa ndio msimamizi na mtoa vibali vyote, sasa wanapopinga agizo la Serikali wanatarajia nini,wakiendelea kukiuka agizo hilo maana yake wanakiuka sheria za nchi,” alisema Kiganja.

Akitolea ufafanuzi suala hilo, Kiganja alisema vyama hivyo  vinapaswa kwenda kusajili jina la biashara kwa  Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), baada ya hapo mhusika anapaswa kuwa na leseni inayotambulika na halmashauri husika.

“Baada ya kuwa na leseni, sasa anatakiwa asajiliwe na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kupatiwa namba ya utambulisho, kisha mhusika anatakiwa asajiliwe na mamlaka ya kisheria iliyowekwa kuratibu shughuli zake ambayo sisi Serikali tunaitambua kuwa ni TPBC,” alisema.

Aidha, Kiganja aliongeza kuwa, vyama na mashirikisho vinapaswa kutekeleza agizo hilo ili viweze kuchangia pato la taifa kwa kulipa kodi.

“Kama wataendelea kukiuka agizo hili, sijui watakuwa wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria gani na mimi kamwe siwezi kuongoza watu ambao wanafanya shughuli zao bila kulipa kodi kutimiza agio la Rais John Magufuli,” alisisitiza.

Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TBPO), Shirikisho la Ngumi za Kulipwa nchini (PST) na TPBC Limited vinadai kuwa Kiganja amekiuka  sheria namba 12 ya mwaka 1967.

Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho mwaka 1971 na kusainiwa na Hayati Mwalimu Julius Nyerere, sheria waliyodai inatamka wazi kuwa BMT inapaswa kushughulikia ngumi za ridhaa pekee

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles