24.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

BONDE EYASI WEMBERE LINA DALILI ZA MAFUTA

Na Mwandishi Wetu

KILA dalili zipo kuwa miamba iliyopo  katika Bonde la Eyasi Wembere, hasa kwenye mabonde madogo ya Wembere na Manonga yaliyopo mikoani Tabora, Shinyanga, Singida na Simiyu, inawezekana kuwa na mafuta kutokana na sifa zake za kijiolojia na kijiofizikia.

Hayo yalisemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini (Uganda), Robert Kasande na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini (Tanzania), Dk. Juliana Pallangyo, katika mkutano na wananchi uliofanyika katika Kijiji cha Mwashiku, wilayani Igunga, mkoani Tabora. Ni habari njema sana.

Viongozi hao walitoa kauli hiyo baada ya timu ya wataalamu kutoka Uganda na Tanzania kufanya ziara katika Bonde hilo, hususani mabonde ya Wembere na Manonga na kutembelea miamba inayoonekana katika maeneo ya Sekenke, mkoani Singida na vijiji vya Mwanzugi na Kining’inila mkoani Tabora.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, alisema baada ya kuona dalili hizo, timu hiyo itatoa mapendekezo mbalimbali kwa wataalamu wa Tanzania ili kuweza kufikia lengo la Serikali la kutafiti mafuta katika bonde la Eyasi na Ziwa Tanganyika.

Alisema endapo mafuta yatapatikana yataweza kusafirishwa katika bomba la mafuta linalotoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Aliongeza kuna uwezekano mkubwa wa Tanzania kugundua mafuta katika Bonde hilo, kufuatia nchi nyingine zenye Bonde hilo kama Kenya na Uganda tayari wamegundua mafuta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles