26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Bodi ya BMT yapewa rungu, wachambuzi kupigwa msasa

Na WINFRIDA MTOI, Mtanzania Digital

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa, amewataka viongozi wa Bodi ya Baraza la Michezo la Taifa(BMT), inayoongwa na Leodgar Tenga, kuhakikisha michezo inaendeshwa kibiashara na timu za Taifa zinafanya vizuri katika michuano ya Kimataifa.

Pia ameitaka bodi hiyo kuhakikisha inawaongezea ujuzi wachambuzi wa michezo nchini ili kusaidia katika maendeleo ya sekta hiyo na kupunguza uhaba wa wataalamu hasa makocha.

“Tumezidiwa idadi ya makocha na Burundi na Rwanda, wale wachambuzi wanaotusaidia kwa kuwa maoni yao huwa tunayachukua na kuyafanyia kazi, tunaomba waongezewe ujuzi ili kupata makocha na wataalamu wa michezo mbalimbali,” amesema.

Mchengerwa ameyasema hayo leo Aprili 20, 2022 wakati akizindua bodi hiyo ya 15 kwenye hafla iliyofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Waziri huyo amesema Serikali inataka kuona matokeo katika utekelezaji wa majukumu iliyopewa bodi hiyo, ikiwamo timu za Taifa kushiriki mashindano ya dunia.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa(katikati) akikabidhi moja ya kitendea kazi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya BMT, Leodigar Tenga(kushoto).

Aidha ameitaka bodi kuimarisha usimamizi wa fedha za mfuko wa maendeleo ya michezo kwa kuhakikisha timu za Taifa zinahudumiwa na miundombinu inaboreshwa.

“Serikali inataka kuona matokeo, nyakati ni tofauti. Niwaambie tu wazi kuwa amkuteuliwa kwa bahati mbaya, nyie ni watu wabobezi, kama hamkuwa na baraka huko nyuma sisi tunawapa baraka zote kushauri vyama na mashirikisho ya michezo,” amesema.

Aidha ametaka kudumishwa kwa utawala bora na utendaji kuanzia ngazi za klabu kwa kuzingatia kanuni, taratibu na viongozi kuacha ubabe na upendeleo.

“Siku nikisikia kuna timu wachezaji wake wamechaguliwa kwa upendeleo na kuwaacha wale wanaostahili, nitakwenda mwenyewe ‘Airport’ kuwarudisha,” ameeleza Waziri huyo.

Kwa upande wake Tenga amemshukuru Waziri Mchengerwa kwa kumuamini na kumhakikishia kutekeleza maagizo yake kwa mujibu wa kanuni.

Naye Ally Mayay ambaye ni miongoni mwa wajumbe wa bodi hiyo, amesema uteuzi huo unaonesha jinsi gani Serikali imemthamini na kuahidi kutoa mchango wake kama inavyotakiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles