22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati yabaini madudu fedha za CSR Tarime

Na Shomari Binda, Musoma

KAMATI iliyoundwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi kuchunguza fedha za CSR zinazotolewa na mgodi wa Barrick North Mara kwa ajili ya miradi ya kijamii imebaini matumizi mabaya ya fedha hizo.

Akizungumza Aprili 20, 2022 kwenye kikao cha wadau wa maendeleo baada ya kupokea taarifa ya uchunguzi wa kamati hiyo, Hapi amesema fedha hizo ni za umma na kila aliyeshiriki kwenye matumizi yake atachukuliwa hatua za kisheria.

Amesema mkoa hauwezi kuona na kukubali kuendelea kufanyika kwa matumizi ya ovyo ya fedha hizo na kwamba kuanzia sasa matumizi yake yatakuwa yakisimamiwa na wahusika kutoka serikalini.

Hapi amesema wapo viongozi ambao wametajwa na kamati hiyo kwa majina kuhusika na matumizi ya fedha hizo na kuagiza jeshi la polisi na TAKUKURU kuwafungulia majarada ya uchunguzi.

Mkuu hiyo wa mkoa amesema fedha hizo za uwajibikaji kwa jamii sio hisani na lazima migodi yote mkoa wa Mara itekeleze wajibu kwa mujibu wa sheria.

“Niwashukuru kamati kwa kazi kubwa mlioifanya licha ya changamoto kubwa mliopitia katika kuifanya kazi hii, hii in vita kwa kuwa yapo masrahi ya watu binafsi yaliyokuwa yakipatikana kupitia fedha hizo na sasa wanakwenda kuzikosa,” amesema Hapi.

Amesema kuanzia sasa ameivunja rasmi kamati ya CDC iliyokuwa ikihusika na ugawaji na matumizi ya fedha hizo na kurudisha usimamizi kwenye halmashauri.

Wakati wa kuwasilisha taarifa yake, kamati imeomba kuzingatiwa mapendekezo ya kamati na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wahusika wa ubadhilifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles