25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mamilioni ya Biko yatua kwa Saida wa Mbagala

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkazi wa Mbagala, jijini Dar es Salaam, Saida Chitime, amefanikiwa kushinda Sh milioni 10 kutoka kwenye droo kubwa ya Biko iliyochezeshwa Sikukuu ya Pasaka na kukabidhiwa fedha zake jana jijini hapa.

Balozi wa Biko Kajala Masanja akionyesha pozi na tabasamu pana wakati anamkabidhi fedha zake Sh Milioni 10 mshindi wao wa Mbagala, Saida Chitime, alizoshinda mwishoni mwa wiki. Picha na Mpiga Picha Wetu.

Akizungumza katika makabidhiano ya fedha zake, Sauda aliishukuru Biko kwa kumkabidhi fedha zitakazoweza kubadilisha maisha yake, akiamini kuwa mchezo huo ni fursa nzuri kwa Watanzania wote wenye nia ya kuondoka kwenye mkwamo kimaisha.

Amesema fedha hizo atazitumia vizuri ikiwa ni pamoja na kuanzisha ujenzi wa nyumba yao iliyokwama kwa siku nyingi kutokana na kukosa pesa, licha ya kumiliki kiwanja jijini Dar es Salaam, huku akisema ni rahisi kucheza Biko kwa kuingia live www.biko.co.tz au kwa namba ya Kampuni 505050 na 2456 namba ya kumbukumbu.

“Biko ni mchezo ambao nimekuwa nikiona watu wanashinda, hivyo nikaamua kuingia kucheza ili nishide kama wenzangu jambo ambalo Mungu amenisaidia leo kukabidhiwa pesa hizi. Nawaomba Watanzania wote wacheze Biko ili nao wajibukulie zawadi za fedha,” amesema Sauda.

Meneja Uhusiano wa Bank ya CRDB tawi la Premier lililopo Palm Beach, jijini Dar es Salaam, Samia Karim, akiwa na mshindi wa Sh milioni 10 wa Biko, Saida Chitime, mwenye maskani yake Mbagala, jijini Dar es Salaam wakati akimkabidhi fedha hizo tayari kuziingiza kwenye matumizi yake. Picha na Mpiga Picha Wetu.

Mbali na wanaocheza kwa kupitia www.biko.co.tz, pia wanaotumia simu za kawaida nao wataendelea kucheza kama zamani kwa kutumia namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu namba 2456 na wote kujishindia kuanzia Sh 2500 hadi Sh milioni tano papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa zinazofanyika kila Jumapili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles