Birdman, Lil Wayne wairudisha YMCMB

0
853

birdman na lil-wayneNEW YORK, MAREKANI

WAKALI wa muziki nchini Marekani, Bryan Williams ‘Birdman’ na Dwayne Carter ‘Lil Wayne’, wamemaliza tofauti zao na wamerudisha kundi lao la Young Money Cash Money Billionaire ‘YMCMB’.

Wawili hao walikuwa kwenye mgogoro uliowatenganisha ambao ulizua maneno mengi kwa mashabiki wao, huku kila mmoja akitupiwa lawama za usaliti kwa mwenzake.

Lakini sasa wapo pamoja wanaendelea na kazi zao katika kundi hilo, huku wasanii wengine kwenye kundi hilo kama Drake, Nick Minaj wakifurahishwa na  mabosi hao kumaliza tofauti zao.

Hata hivyo, Lil Wayne ataendelea kudai fedha zake kwa Birdman, dola milioni 51 ambazo ndizo zinazodaiwa kusababisha tofauti zao.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here