23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Buffon atangaza kustaafu soka

buffonTURIN, ITALIA

MLINDA mlango wa timu ya Taifa ya Italia na klabu ya Juventus, Gianluigi Buffon, ametangaza kustaafu soka baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018, ambayo itafanyika nchini Urusi.

Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 37, anajivunia kuwa na mafanikio makubwa ya kuchukua ubingwa wa Kombe hilo mwaka 2006, akiwa na timu yake ya Taifa, huku akichukua ubingwa wa Ligi Kuu nchini Italia mara sita akiwa na klabu hiyo ya Juventus.

Hata hivyo, mchezaji huyo amedai kwamba ifikapo mwaka 2018 atawapisha walinda milango wengine kwa ajili ya kuendelea kutoa mchango wa kuisaidia timu ya Taifa na klabu.

“Lengo langu ni kujaribu kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya mwisho na ndipo utakuwa ni wakati wangu wa kufunga mlango katika mchezo wa soka na kuwapisha walinda milango wengine wajitolee kwa ajili ya Taifa na klabu,” alisema Buffon.

Hata hivyo, mlinda mlango huyo amedai kwamba alistahili kuwa katika kinyang’anyiro cha tuzo ya Ballon d’Or, lakini anaamini asingeweza kutwaa taji hilo.

“Nilistahili kuwa katika orodha ya kuwania tuzo ya Ballon d’Or, lakini nilikuwa najua kwamba siwezi kushinda mbele ya wachezaji wale hatari na kama ningechukua basi lingekuwa ni jambo la kushangaza,” aliongeza.

Klabu ya Juventus kwa sasa inaendelea kufanya vizuri katika msimamo wa Ligi ambapo inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 45 baada ya kucheza michezo 21, huku Napoli ikiwa na alama 47, ikiongoza Ligi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles