27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serena atinga nusu fainali Australia Open

SERENA WILLIAMSMELBOURNE, AUSTRALIA

NYOTA wa mchezo wa tenisi, Serena Williams, amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali katika michuano ya wazi ya Australia, baada ya kumchapa mpinzani wake, Maria Sharapova kwa seti 6-4, 6-1.

Serena amekuwa mwiba kwa mpinzani wake huyo kwa kuwa ni ushindi wake wa 14 mfululizo kumshinda Sharapova katika michuano hiyo.

Hata hivyo, Serena ni bingwa mtetezi wa taji hilo, huku ikiwa analisaka kwa mara ya 22 kwenye michuano ya Grand Slam, mchezo huo wa robo fainali kwenye uwanja wa Melbourne Park.

Imepita miaka 12 sasa tangu nyota huyu wa nchini Marekani alipopoteza mchezo dhidi ya Sharapova, Serena atachuana na Agnieszka Radwanska katika hatua ya nne bora.

Hata hivyo, Serena ametamba kufanya vizuri katika michuano hiyo na kuchukua ubingwa, japokuwa kuna ushindani mkubwa dhidi ya wapinzani wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles