23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Xavier awa kocha mpya Msumbiji

Gil Vicente vs OlhanenseMAPUTO, MSUMBIJI

NYOTA wa zamani wa klabu ya Liverpool, Abel Xavier, ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Msumbiji.

Xavier, ambaye ana umri wa miaka 43, aliwahi kukipiga katika klabu ya Everton, LA Galaxy ya nchini Marekani na timu ya Taifa ya Ureno, huku akicheza nafasi ya ulinzi.

Xavier alizaliwa nchini Msumbiji, lakini alihamia Ureno huku akiwa na umri mdogo na kufanikiwa kuitumikia timu hiyo ya Taifa kwa kucheza michezo 20, lakini kwa sasa amefanikiwa kuwa kocha mpya wa timu hiyo.

“Nina furaha kubwa kuteuliwa kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Msumbiji, hii ni nchi yangu kwa kuwa nilizaliwa hapa na sasa nimerudi tena kwa ajili ya kulitumikia taifa,” alisema Xavier. 

Kocha huyo aliwahi kuitumikia klabu ya Everton na kuichezea michezo 49 kabla ya kujiunga na Liverpool mwaka 2002 kwa kitita cha pauni 800,000.

Hata hivyo, kocha huyo amedai kwamba ana kazi kubwa ya kuisaidia timu hiyo katika michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2017, huku timu hiyo ikiwa mara ya mwisho kushiriki michuano hiyo ilikuwa mwaka 2010.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles