Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, alisajiliwa na Chelsea kutoka Benfica mwaka 2010 kwa pauni milioni 17, wakati huo klabu hiyo kutoka China imeweka mezani kitita cha pauni milioni 25 kwa ajili ya kumnasa nyota huyo.
Ramires alisaini mkataba mpya na klabu yake wa miaka minne Oktoba, mwaka jana, ila alipata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza katika michezo saba tu msimu huu wa Ligi Kuu nchini England.
Timu ya Jiangsu ilimaliza katika nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi msimu wa mwaka 2015, huku kikosi hicho kikiwa kinanolewa na nyota wa zamani wa Chelsea, Dan Petrescu.
Kiungo huyu wa Kibrazil akiwa na The Blues, ametoa mchango mkubwa wa timu hiyo kutwaa mataji mbalimbali kama vile Ligi Kuu, Kombe la FA, ubingwa wa klabu bingwa Ulaya na ile michuano ya Europa.