Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WAENDESHAJI wa bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, jana wamemkabidhi Sh milioni 20, mshindi wa droo ya 28, Moses Matagili, mkazi wa Goba, aliyetangazwa juzi Dar es Salaam.
Matagili anakuwa mshindi wa droo ya 28 ya Biko, inayochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money, kuanzia Sh 1,000 na kuendelea, huku namba ya kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Matagili, anayejishughulisha na kazi za ujenzi wa nyumba, alisema amepokea ushindi wake kwa furaha, baada ya kuuwazia kwa muda mrefu na kuamua kuwa mchezaji mzuri wa Biko.
Alisema makabidhiano hayo ya fedha yamefanyika haraka, tofauti na matarajio yake, ikiwa ni siku moja baada ya kupigiwa simu ya ushindi na Balozi wa Biko, Kajala Masanja.
“Nashukuru kwa kushinda na kukabidhiwa fedha zangu mapema, nikiamini kuwa nitapiga hatua kubwa kiuchumi kwa namna moja ama nyingine, ukizingatia kuwa ndiyo matarajio yangu.
“Nawaomba Watanzania wote waendelee kucheza Biko mara nyingi zaidi na wasikate tamaa, kwa sababu kushinda kwangu kumeniongezea imani kubwa kwa waendeshaji wa Biko,” alisema.