24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

BEYONCE KUINUNUA HOUSTON ROCKETS

LOS ANGELES, MAREKANI

MSANII wa muziki nchini Marekani, Beyonce Knowles, anataka kuonesha jeuri ya fedha kwa kuinunua timu ya kikapu ya Houston Rockets, ambayo inashiriki Ligi Kuu ya NBA nchini humo.

Mrembo huyo ambaye anakadiriwa kuwa na utajiri wenye thamani ya dola milioni 350  zaidi ya bilioni 775 za Kitanzania, ameweka wazi kuwa yupo kwenye mipango ya kuinunua timu hiyo, baada ya mmiliki wa timu hiyo Les Alexander, kuthibitisha kuiuza.

Timu hiyo imewahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya kikapu nchini humo mara mbili. Alexander aliinunua timu kwa kitita cha dola milioni 85 mwaka 1993 zaidi ya bilioni 188.

Beyonce anataka kufuata nyayo za mume wake, Jay Z, ambaye aliwahi kuwa na hisa katika timu ya Brooklyn Nets, lakini alikuja kuziuza mwaka 2013.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles