25.9 C
Dar es Salaam
Sunday, December 4, 2022

Contact us: [email protected]

NANDY AANZA KUANDAA BORA ZAIDI YA ‘WASIKUDANGAYE’

Na JESSCA NANGAWE-DAR ES SALAAM

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Faustina Charles ‘Nandy’, amesema anaumiza kichwa kuandaa kazi mpya ambayo itakuwa bora zaidi ya ‘Wasikudanganye’.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Nandy alisema anajisikia vizuri kuona kazi zake zikizidi kukubaliwa na mashabiki, hali inayompa nafasi ya kujipanga upya kufanya wimbo bora zaidi.

 “Nimekua na mapokeo mazuri ya kazi zangu kwa mashabiki, hii inanipa moyo wa kuzidi kufanya vizuri zaidi, najua wimbo wangu wa ‘Wasikudanganye’ umeendelea kufanya vema,” alisema Nandy.

Nandy amekua miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri hapa nyumbani na kukubalika kwa mashabiki kutokana na aina ya nyimbo anazoimba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,538FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles