KATIKA hotuba yake jioni ya jana, Rais wa Marekani, Joe Biden, amesema jeshi la nchi hiyo liko kwenye maandilizi ya kushambulia maeneo na mali za Kundi la IS.
Onyo la Biden linakuja baada ya matukio mawili ya kushambuliwa kwa Uwanja wa Ndege wa Kabul nchini Afghanistan, ambapo wanajeshi 13 wa Marekani waliuawa.
Baada ya shambulio hilo lililosababisha raia wa Afghanistan 95 kupoteza maisha, Kundi la IS la Afghanistan lilikiri kuhusika huku likidai litaendeleza matukio ya aina hiyo dhidi ya Marekani na washirika wake.
Akijibu hilo katika hotuba, Biden amesema: “Hatutishwi na magaidi. Hatutaacha wazuie mipango yetu… Hatutawasamehe, hatutawasahau. Tutawaangusha, lazima mtajuta.”