27.9 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Moto kambi ya jeshi waua tisa

MOTO uliozuka kwenye kambi ya jeshi Kusini mwa Kazakhstan umeua wanajeshi tisa na kujeruhi watumishi wengine 90, kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo.

Katika tukio hilo la mjini Jambyl, taarifa zaidi zinadai kuwa wanajeshi hao walifariki wakati wakijaribu kuzima moto huo ulioambatana na milipuko.

Kwa mujibu wa mamlaka za mjini Jambyl, kati ya watu 90 waliokuwa wamejeruhiwa, 28 walilazwa hospitali, huku wengine sita wakiwa kwenye hali mbaya zaidi.

Wakati huo huo, watu zaidi ya 1,000 wanaoishi karibu na kambi hiyo wamehamishiwa kwingineko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles