23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi wanasa ndizi zinazosafirisha ‘unga’

POLISI nchini Montenegro wamethibitisha kukamata kilogramu 907 ya dawa za kulevya aina ya Cocaine zilizokuwa zimefichwa ndani ya meli ya kusafirisha ndizi.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, watu wawili wanashikiliwa wakihusishwa na dawa hizo zilizokuwa zimetengwa katika mafungu 1,250.

Aidha, huku hicho kikiwa ni kiwango kikubwa zaidi cha unga kuwahi kukamatwa nchini humo, Naibu Waziri Mkuu, Dritan Abazovic, amejitokeza kupongeza kazi iliyofanywa na vyombo vya usalama.

“Ni kazi nzuri ya polisi wa Montenegro. Tunafanya kile tulichopania, kwamba Montenegro haiwezi kuwa nchi ya uhalifu,” amesema kiongozi huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles