MABOSI wa PSG wameendeleza fujo zao kwenye soko la usajili kwa kuanza kuifukuzia saini ya mpachikaji mabao hatari wa Borussia Dortmund, Erling Haaland.
Hatua yao hiyo inakuja zikiwa ni wiki chache tu zimepita tangu walipoutikisa ulimwengu wa soka kwa kumsajili mkali wa mabao, Lionel Messi.
Aidha, huku Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi, akisema hawana mpango wa kumsajili Cristiano Ronaldo, imefichuka kuwa wamehamishia nguvu kwa Haaland na kiungo wa Manchester United, Paul Pogba.
Harakati za klabu hizo zinalenga kuziba pengo la Kylian Mbappe ambaye anaweza kwenda Real Madrid kabla ya kufungwa kwa usajili huu wa kiangazi Agosti 31, mwaka huu.