24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Betty kufuata nyayo za Shusho

BETTYNA GEORGE KAYALA

MWIMBAJI chipukizi wa muziki wa injili kutoka nchini Kenya, Betty Chepkorir, amesema kwamba ndoto zake ni kufuata nyayo za mkali wa muziki huo, Christina Shusho ambaye nyimbo zake zimekuwa zikiwagusa mashabiki wengi wa muziki huo nchini Kenya.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Betty aliyekuwa nchini kwa ziara ya muziki kwa muda wa wiki moja na kufanikiwa kurekodi video ya wimbo wake uitwao ‘Nifanye Wako’, alisema kwa muda mrefu amekuwa akisikiliza nyimbo za Shusho kitendo kilichopelekea naye avutiwe kuimba nyimbo za injili.

“Nafuata nyayo za Shusho, nyimbo zake zimenifanyia baraka katika maisha yangu, kwani zina mguso wa hali ya juu nami natamani niwe na utunzi kama wake ili nifikishe ujumbe wa Mungu katika jamii kwa njia hiyo ya uimbaji,” alisema Betty.

Mbali na uimbaji, Betty pia ni mwigizaji wa maigizo ya jukwaani akiwa chini ya kampuni ya Afrika Nasaha Production ya nchini Kenya inayofanya kazi kwa ushirikiano na 5 Effects Movies Ltd ya jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles