MKALI wa hip hop nchini Marekani, Jay Z na mke wake Beyonce, inadaiwa kuwa wanatarajia mtoto wao wa pili.
Habari hizo zimeenea baada ya wawili hao kuonekana wakitoka kwenye tuzo za Golden Globes mwanzoni mwa wiki hii huku Beyonce akiwa amevaa nguo ambayo inazuia tumbo lake kuonekana.
Kutokana na hali hiyo, watu mbalimbali wanaamini kuwa msanii huyo ana ujauzito hivyo hataki watu waone ukubwa wa tumbo hilo.
Wawili hao kwa sasa wana mtoto mmoja ambaye ni wa kike mwenye umri wa miaka minne anajulikana kwa jina la Blue Ivy Carter. Hata hivyo, Beyonce hajaweka wazi kama kweli ana ujauzito kama watu wanavyodhani.