BEI ya korosho kwenye mnada katika  maghala ya Chama Kikuu cha Mwambao Lindi,imepanda hadi Sh 3,810 kutoka Sh 3,710 kwa kilo katika mnada wa kwanza.
Hayo yamejitokeza kwenye  mnada wa korosho uliofanyika katika Chama cha Ushirika Tapwa wilayani kilwa mkoani Lindi jana.
Akizungumzia hali hiyo,Meneja wa Chama Kikuu cha Kuuza na Kununua Mazao Mwambao, Hasan Vudu alisema tani 2,355 za korosho zimeingizwa kwenye mnada na makampuni zaidi ya 19 yalishiriki kwenye zabuni
Vudu.
Alisema ushiriki mzuri wa makapuni kwenye minada unachangia kuwapo bei mzuri ya korosho kwani unaleta ushindani Kwenye soko.
Kwa upande wake, mkulima Mohamedi Ismail mkulima alisema bei ya korosho sasa inatia moyo na kurudisha matumaini kwa wakulima na kuongeza mori ya kufufua mikorosho iliyokufa kuhudumia na kupanda   mipya.
Alisema ni wajibu wa wadau wa korosho,wakiwamo Bodi ya Korosho na Mfuko wa Kuendeleza zao hilo (WFU), kusimama imara
Kwa upande wake, Sharifa Mokiwa kutoka Bodi ya Korosho,aliwataka wananchi na wakulima wa korosho kukausha korosho zao ili kupunguza unyevu ambao unaweza kusababisha zao kupunza ubora na uzito wa korosho.