31.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

‘Pelekeni watoto wakajisomee maktaba’

maktabaNA FLORENCE SANAWA, MTWARA

WAZAZI mkoani Mtwara,wametakiwa kutoa hamasa kwa watoto wao ili kutumia huduma za maktaba kutokana na kuwapo mwitiko mdogo wa kujisomea hatua.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Khatibu Kazungu wakati akifugua mafunzo ya siku moja yaliyoandaliwa na Bodi ya Maktaba Kuu Tanzania katika mradi wa ‘Library for Development’ kwa ushirikiano wa maktaba kutoka nchini Finland.

Alisema ili Taifa liwe na mabadiliko lazima kuwe na lengo la kuboresha huduma za maktaba na kuleta nyenzo muhimu ili kuweza kukidha mahitaji ya wananchi na Taifa kwa ujumla katika kujisomea.

Alisema wananchi wanapaswa kutumia vema huduma hizo ili kupata mafunzo ya Tehama ikiwa ni sehemu ya kujifunza mbinu mpya katika biashara ili waweze kunufaika.

“Unajua nchi zilizoendelea,ikiwamo Finland zimekuwa na mtokeo mazuri ya shule kutokana na huduma bora za maktaba,tunapaswa kuchukua hatua za makusudi  kuhamasisha wazazi ili  watumie nafasi hiyo kuelimisha  watoto wao wajiendeleze kwa kusoma vitabu, majarida sambamba na kutumia  mitandao ya kijamii ili kuongeza ujuzi na maarifa” alisema  Dk. Kazungu

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Maktaba,Dk. Alli Mcharazo alisema wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kwa ajili ya maendeleo na kuwajengea uwezo wasomaji na jamii inayowazunguka ili kuweza kumaliza matatizo mbalimbali ili kuweza kuyatatua kwa teknolojia mpya.

Alisema zipo juhudi mbalimbali ambazo bodi ya maktaba,imekuwa ikifanya ili kuwafikia watu mbalimbali kwa kufanya  matamasha na kuhamasisha watu kusoma huku wanafunzi wakitembelewa mashuleni.

“Tukiwa na vifaa vya kutosha tunaweza kwenda mojamoja kwa wananjamii ili kuongeza mwamko wa kutumia huduma za maktaba mbalimbali zikiwemo kwenye taasisi,shuleni na zile za umma ili kuhamasisha usomaji pamoja na watu wengi kutumia mitandao kujisomea zaidi” alisema Dk.Mcharazo

Kwa upande wake, Mkutubi Maktaba ya Mkoa wa Mtwara Fredy Mpoma alisema mradi wa ‘Library for Development,’ umeanza kutekelezwa mwaka huu,lakini mwamko ni mdogo hali ambayo inalazimu wafanyakazi wa maktaba hiyo kutembelea maeneo mbalimbali ili kutoa elimu ya matumizi ya  huduma za maktaba.

“Tumekuwa tukitumia muda mwingi kutoka ndani ya maktaba ili kuweza kuhamasisha jamii iweze kutumia huduma za maktaba pamoja na kufanya hamasa mbalimbali bado mwamko uko duni sana, lakini tunapata ahueni baada ya kuona watoto wa shule za msingi wakifika japo ni kwa uchache sana” alisema Mpoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,586FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles