33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Basi la Kilimanjaro lapinduka

OSCAR ASSENGA-HANDENI

ZAIDI ya abiria 52 waliokuwa wamepanda basi la Kilimanjaro kutoka jijini Arusha kuelekea Dar es Salaam, wamenusurika kifo baada ya basi hilo kuacha njia na kupinduka eneo la Mkata, wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe, alithibitisha kutokea ajali hiyo na kusema ilitokea jana saa tisa mchana, baada ya basi hilo kuteleza na dereva kushindwa kulimudu.

“Inaonekana basi lilipoteleza, dereva ambaye hadi sasa jina lake halijafahamika kwa sababu ana hali mbaya, alishindwa kulimudu na hivyo kupinduka.

“Pamoja na hayo, waliojeruhiwa ni abiria 18 na sita kati yao, walipata majeraha makubwa na kulazimika kupelekwa kwenye Kituo cha Afya Mkata kwa ajili ya matibabu zaidi.

“Kati ya majeruhi hao, wanawake ni 15 na wanaume ni watatu,” alisema Kamanda Bukombe.

Wakati huo huo, Kamanda Bukombe aliwataka madereva kuwa makini pindi wanapokuwa barabarani hasa katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha.

“Katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha, lazima madereva wawe makini barabarani kwa sababu magari yanaweza kupoteza mwelekeo wakati wowote kutokana na utelezi wa barabarani.

“Pamoja na hayo, lazima wazingatie sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kutoendesha kwa mwendo kasi, kwani mwendo kasi siku zote una madhara makubwa yakiwamo kusababisha vifo, ulemavu na uharibifu wa mali za abiria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles