23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Ndungulile: Wanasiasa acheni kuingilia taaluma ya afya

DERICK MILTON-BARIADI

NAIBU Waziri ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile, amesema wizara hiyo imechoshwa na baadhi ya viongozi wakiwemo wanasiasa ambao wamekuwa wakiingilia taaluma ya afya bila ya kufuata utaratibu.

Kutokana na hali hiyo, alisema  wizara haiko tayari kuona hali hiyo ikiendelea, huku akiwataka wanasiasa kuacha wataalamu hao wa afya watimize majukumu yao.

Hayo aliyasema jana mjini Bariadi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wakunga duniani ambazo kitaifa zimefanyikia mkoani Simiyu.

Alisema anashangazwa na watu hao ambao wamekuwa kila mara wakiingilia taaluma yao bila ya utaratibu na kutoa maneno na maagizo yanayokiuka sheria za kazi yao.

Alisema watu hao wamekuwa wakiingilia taaluma ya afya pekee bila ya kuingilia taaluma nyingine, ambapo aliwataka kuacha mara moja na kuwaachia wataalamu kufanya kazi zao kwa ufasaha.

“Masuala ya kitaaluma yaachwe kwa wanataaluma, sekta ya afya imeanza kuingiliwa sana, kila siku utasikia hili na lile, tuacheni wenyewe tufanye kazi kitaaluma,” alisema Dk. Ndungulile.

Alisema ni vizuri viongozi kuwasiliana na viongozi wa wizara kabla ya kuingilia jambo lolote kwenye idara hiyo, huku akiwataka kutumia zaidi mabaraza ya wafanyakazi katika kutatua jambo.

“Masuala ya kitaalamu yaacheni yatatuliwe kitaalamu, tumechoka na kuingiliwa, kama kuna tatizo wasiliana na sisi kwanza wizara au tumieni mabaraza ya wafanyakazi, sekta hii imeingiliwa sana sasa inatosha,” alisema Dk. Ndungulile.


Naibu Waziri ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo alisema Serikali haijakataza watu kuendelea kuzaa ila inasisitiza watu wazae watoto watakaoweza kuwalea.

Aliwataka wanaume nchini kwenda na wake zao kliniki pindi wanapopata ujauzito ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na vifo vya mama na mtoto.

Alisema Serikali itaendelea kuajiri wakunga zaidi ili kufikia lengo la kuwa na wakunga 100,000, ambapo waliopo ni wakunga 47,870 huku mahitaji yakiwa ni 52,130.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), Freddy Mwanga, alisema chama hicho kimesikitishwa na tamko la Serikali lililotolewa hivi karibuni juu ya kupunguzwa kwa sifa za kujiunga na ukunga.

Alisema kitendo hicho kitaathiri sana ukuaji wa taaluma yao ya uuguzi kutokana na kutompatia mkunga nafasi ya kujiendeleza katika vyuo vya elimu ya juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles