22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Bashungwa, Kichere kuapishwa kesho

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais Dk. John Magufuli anatarajia kuwaapisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Charles Kichere kesho Jumatatu Juni 10, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo inatokana na mabadiliko madogo ya mawaziri ambapo alitengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda na kumteua Bashungwa ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Pia Rais Magufulu alitengua uteuzi wa Kichere aliyekuwa Kamishna Mamlaka ya Mapato (TRA), ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Njombe.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu leo Jumapili Juni 9, imesema pia imesema baada ya Rais kuwaapisha viongozi hao atashuhudia tukio la Kampuni ya Bharti Airtel International kutoa mchango wa Sh bilioni mbili na milioni 270 ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles