22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Pacha waolewa na pacha Uganda

ENTEBE, UGANDA

MAPACHA Priscilla Babirye na Pereth Nakato mabinti wa marehemu Kaddu Ssalongo kutoka kijiji Rugando nchini Uganda wamepata wenza ambao ni mapacha na hicho ndicho ambacho kimeshangaza wengi.

Mabwanaharusi  hao mapacha, Asiimwe Edward mfanyabiashara katika mji wa Mbarara mashariki mwa Uganda na Amos Besigye Kutoka wilaya ya Ntungamo ambaye ni mvuvi katika wilaya ya Rwampara wanatoka katika familia tofauti na walikutana na mabinti hao katika tukio moja lakini kwa nyakati tofauti.

Besigye anasimulia kuwa safari yao ya mapenzi kuwa ilianzia msibani wakati alipokwenda kumfariji bwana mmoja na Nakato na pacha wake  nao walikuwa wamekwenda kuifariji familia hiyo hiyo.

Anasema wakati ameketi kwenye hema kama mgeni, mbele yake alimuona msichana mrembo akiwa amesimama akipigwa na jua ndipo alipomuita na kumuomba waketi pamoja.

Ghafla anasema alishangaa kumuona msichana mwigine kama yeye akiwa amesimama mahali pale alipokuwa amesimama.

Anasema mtu mmoja alimwambia ni mapacha hivyo ilibidi avute kiti kingine ili akae nao wote wawili. 

Baadae alimuomba namba za simu rafiki yao ili awatumie ujumbe na kubaini kuwa Nyakato alikuwa akifanya kazi katika duka la dawa karibu na nyumbani  kwao na hapo ndipo mazoea na kukutana kwao kulipoanza.

Nyakato kwa upande wake anasema mara baada ya kukutana kwenye msiba baadae alipokea jumbe za simu na hakuzijibu kwa sababu yeye na pacha wake walikubaliana tangu zamani wakiwa shule ya msingi  kuolewa siku moja. 

Anasema pacha wake alipomwambia anachumbiwa na mwanamme, ilinibidi awe makini pia.

Babirye yeye kwa upande wake anasema mume wake huyo walisoma wote chuo cha Trinity wilayani Kabale na hawakuwahi kuzungumza.

Lakini siku hiyo hiyo wakati wanatoka kwenye mazishi akiwa na pacha wake wakakutana na Edward na kumuomba namba ya simu na kumpatia na baadae akaanza kumwambia maneno matamu.

Anasema alimshirikisha pacha wake juu ya jumbe alizokuwa akimtumia na yeye alimwambia  jinsi walivyokutana na Besigye kwenye mazishi hay ohayo.

Edward kwa upande wake anasema alipoanza kumpigia simu Babirye alionekana kama hajali lakini yeye alitamani kuoa pacha kwa sababu na yeye pia ni pacha kwa hiyo hakutaka tamaa na kujaribu bahati yake.

Besigye anasema wakati mambo yalipofika mbali mabinti hao mapacha waliomba wote wakutane pamoja na kubadilishana mawazo juu ya maisha yao na baadae walifikia mipango ya ndoa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles