26.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) lajipanga kusimamia miradi ya ujenzi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Baraza la Wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), limesema linakabiliwa na upungufu wa wafanyakazi hali inayopelekea kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Hayo yameelezwa leo Alhamis Desemba 17, na Mtendaji Mkuu wa NCC, Dk. Matiko Mturi, kwenye kikao cha siku mbili cha baraza hilo.

Amesema katika mwaka wa fedha 2020/21 baraza linao wafanyakazi 30 kati ya 83 wanaohitajika ili kuliwezesha kutekeleza majukumu yake ya kisheria iapsavyo.

Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi(NCC), Dk. Matiko Mturi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano mpango kazi wa Wafanyakazi uliofunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi Elius Mwakalinga uliofanyika Dar es Salaam.

“Changamoto hii imetokana na baadhi ya wafanyakaziwa baraza kuondoka katika utumishi wa umma kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kustaafu utumishi wa umma na wengine kuhamia kwenye taasisi nyingine.

“Hii inafanya baraza kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo, pia uhaba wa wafanyakazi wenye sifa za stahili umesababisha baraza kushindwa kujaza nafasi za wakuu wa idara kwa muda mrefu,” amesema Dk. Mturi.

Aidha, ameitaja changamoto nyingine kuwa ni ufinyu wa bajeti ambayo amesema inasababisha baraza kushindwa kutekeleza majukumu yake ya msingi kwa kiwango kinachostahili opamoja na kushindwa kulipia stahiki za wafanyakazi kwa wakati.

“Changamoto hii inasababisha upungufu na uchakavu wa vitendea kazi kutokana na NCC kushindwa kukarabati au kununua vitendea kazi vipya.

“Uhaba huu unasababisha NCC kujielekea katika kufanya kazi za Consultancy nyingi ili iweze kuongeza kipato kwa ajili ya kugharamia mahitaji yake ya msingi badala ya kutekeza majukumu mengine ya msingi ambayo yanahitaji fedha,” amesema Dk. Mturi.

Amesema mkakati uliopo sasahivi ni kuendelea kuhuisha Baraza la Taifa la Ujenzi kwa kuliongezea uwezo wa kisheria ili liweze kuratibu ipasavyo maendeleo ya sektabya ujenzi pamoja na kuwa na vyanzo endelevu vya mapato.

Katika mwaka huu wa fedha 2020/21 NCC imejipanga kuhakikisha kuwa inakusanya taarifa zinazohusu bei za vifaa vya ujenzi katika mikoa yote ikiwamo kuandaa muongozo wa mabadiliko ya gharama za ujenzi kwa kila mwezi.

“Pamoja na hayo pia, kutoa mafunzo kwa wadau wa sekta ya ujenzi , kuratibu usuluhishi wa migogoro inayotokea katika sekta ya ujenzi, kutoa ushauri wa kitaalamu wa sekta hii na kutekeleza ukaguzi wa utekezaji wa miradi inayofadhiliwa na mfuko wa barabara katika mkoa wa Morogozo,” amesema Dk. Mturi.

Upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Elius Mwakalinga amesema amepokea changamoto hizo na kwamba atazifanyia kazi huku akiwataka kuwa wabunifu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi Elius Mwakalinga akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wafanyakzi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) uliofnyika Dar es Salaam

“Nimesikiliza changamoto zenu na niwaahidi tu kwamba nitazifanyia kazi kwa haraka sana, lakini pia niwatake muwe wabunifu kwenye shughuli zenu na mtumie muda wenu mwingi kutembelea miradi ili mjifunze na kujua kinachoendelea huko kuliko kukaa ofisini na kusubiri taarifa ambazo wakati mwingine hazina uhalisia,” amesema Mhandisi Mwakalinga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles