29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Afisa ardhi jela kwa kugushi nyaraka

Na Samwel Mwanga, Simiyu

Mahakama ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imemhukumu aliyekuwa Afisa Ardhi wa wilaya hiyo, Octavian Mishana kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya Sh 600,000 kwa kosa la kughushi nyaraka.

Hukumu hiyo imetolewa jana na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo,Enos Misana baada ya mshitakiwa kuomba kukiri kosa linalomkabili mbele ya mahakama hiyo.

Mara baada ya mshitakiwa kukiri makosa yake mwendesha mashitaka wa serikali,Rehema Sakafu aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Kabla ya mahakama kutoa hukumu hiyo mshitakiwa aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ana umri mkubwa, ni mgonjwa wa kisukari na ni mkosaji wa mara ya kwanza.

Awali, ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha mashitaka huyo kuwa  mshitakiwa alifikishwa mahakamani hapo Septemba 19, 2019 kwa kosa la kughushi stakabadhi ambazo alidai ni za halmashauri hiyo huku akifahamu si kweli na kukusanya kiasi cha fedha Sh 1,192,000 kwa ajili ya kupima viwanja na kuzitumia kwa matumizi yake binafsi.

Mwendesha mashitaka alizidi kuieleza kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kati ya mwaka 2002 hadi 2007 akiwa Afisa Ardhi wa wilaya hiyo kabla ya kuhamishiwa  wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera ambapo kwa sasa amekwisha kustaafu kazi serikalini.

Amesema kuwa kosa hilo ni kinyume  na kifungu 333, 335 na 337 vya sheria ya kanuni ya adhabu. Hata hivyo mshitakiwa aliweza kulipa faini hiyo na kukwepa kwenda jela na hivyo kuachiwa huru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles