25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Tawla Arusha yakutananisha waangalizi wa Uchaguzi Mkuu 2020

Na Janeth Mushi, Arusha 
 
Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (Tawla), tawi la Arusha, kimekutanisha waliokuwa Waangalizi wa Uchaguzi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu, kujadili na kutoa mrejesho kuhusu uchaguzi huo.
 
Wadau hao walikutana jana jijini Arusha ambao walitokea majimbo ya Longido, Monduli, Karatu, Arumeru Mashariki na Arumeru Magharibi.
 
Tawla ilikutanisha wadau hao kupitia mradi wake wa IDIET ambao wanautekeleza katika mikoa mbalimbali hapa nchini nambao unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
 
Akizungumza katika majadilianao hayo mmoja ya watekelezaji wa mradi huo kutoka Tawla, Clara Chuwa, alisema mradi huo una lengo la kuangalia ushiriki wa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu katika mchakato mzima wa uchaguzi.
 
Alisema katika mradi huo wanashirikiana na Taasisi ya Vijana ya TYC na kuwa moja ya kazi walizofanya ni kuangalia ushiriki wa makundi hayo ambapo mradi huo unatekelezwa katika mikoa ya Mwanza,Tanga na Arusha.
 
“Kwa Arusha umradi  ulikuwa unatekeleza katika wilaya za Arumeru(yenye majimbo mawili), Monduli na Karatu.Tulifanya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile serikali na vyama vya siasa.
 
“Tunashukuru wadau kwani tumeshirikiana na kusaidia kufanikisha lengo zima la mradi ambalo ni kuangalia ushiriki wa walengwa wa mradi,”alisema Clara.
 
Upande wake, Elibariki Laizer ambaye alikuwa mwangalizi wa uchaguzi jimbo la Monduli, amesema uchaguzi huo ulikwenda vizuri na kuwa baadhi ya maeneo yalikuwa na changamoto ndogo ambazo ziliweza kutatuliwa na uchaguzi kuendelea.
 
“Kulikuwa na changamoto kidogo ambazo zilitokea katika vituo ila nyingi ni ndogo ikiwemo wasimamizi wa kata kutotaka tukae kwenye vituo ila alipopita Msimamizi wa Jimbo aliwawataka watuache tubaki na kuangalia zoezi zima la uchaguzi mpaka zoezi la kuhesabu kura.
 
“Kulikuwa na changamoto hasa kwa watu wenye ulemavu hasa wale ambao hawaoni,walikuwa wanakuja na mtu wa kumsaidia kupiga kura ila walikuwa hawaamini kama wanawasadia kuchagua wanaowataka,” amesema Laizer.
 
Nae, Biliuda Kisaka ametaja miongoni mwa changamoto walizobaini kwenye vituo ni pamoja na watu wa makundi maalum ikiwemo walemavu wa viungo,miundombinu kutokuwa rafiki kwao.
 
“Tunaomba serikali itenegneze mazingira mazuri kwa makundi maalum katika chaguzi zijazo ili kuwawezesha kutekeleza haki zao ya msingi ya kikatiba kwani miundombinu katika vituo vingi haikuwa rafiki hasa kwa maeneo ya pembezoni,” amesema Kisaka.
 
Kwa upande wake mwezeshaji wa majadiliano hayo, Firimini Miku amesema katika kikao kazi hicho wadau hao walijadiliana mafanikio, changamoto, maboresho kwa wadau na sekta binafsi na nini kifanyike ili kuboresha changuzi zijazo.
 
“Katika majadiliano haya tumeona bado serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo wana wajibu wa kuendelea kutoa elimu zaidi ya mpiga kura hasa maeneo ya vijijini.
 
“Kwa upande wa vyama vya siasa bado wanahimizwa kutenda haki na kutoa fursa kwa vijana na wanawake katika kuwania nafasi za uongozi,ili kuongeza idadi yao katika ngazi mbalimbali za maamuzi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles