27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Nifty Boi atua Bongo kufanya video ya Different Vibe

Na Jeremia Ernest, Dar es Salaam

Nyota wa muziki nchini Nigeria, Enoch Solomon ‘Nifty Boi,’ ametua Tanzania kwa ajili ya kufanya video ya Different Vibe ambayo ni moja ya ngoma yake iliyopo katika kwenye Albamu fupi (EP) yake ya kwanza.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Desemba 17, amesema amevutiwa na mandhari za hapa nchini ndiyo maana amechagua kuja kufanya video hiyo.

“Tanzania kuna mazingira mazuri ambayo yanapendeza katika video ndio sababu iliyonifanya nije kufanya kazi yangu hapa ukizingatia tasnia yao ya muziki inakua kwa kasi,” amesema Nifty Boi.

Ameongeza kuwa mbali na mazingira Tanzania ni nchi ya amani hakuna malumbano wananchi wake ni wakarimu hivyo ni rahisi katika ufanyaji wa kazi.

Mbali na Nifty Boi kuja kufanya video hapa nchini hivi karibuni msanii mkongwe wa dansi Koffe Lomide naye alikuja Tanzania kwa ajili ya kurekodi video ya nyimbo yake ambayo ameahidi kuitoa siku za usoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles