25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Bandari yatakiwa Kutokomeza ufisadi

Makame MbarawaNA CHRISTINA GAULUHANGA, DAR ES SALAAM

BODI ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imetakiwa kuhakikisha inaifumua upya  bandari hiyo kwa kutokomeza  ufisadi na ajira za kurithishana.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa alikuwa akizungumza   Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa bodi mpya mamlaka hiyo.

Alisema mifumo ya bandari hiyo  na uongozi uliokuwapo ulisababisha bandari   kupoteza mabilioni ya fedha na kuisababishia serikali hasara.

Mbarawa alisema michezo michafu ya kupeana ajira za kurithishana nayo  imekuwa kichocheo cha wafanyakazi wasio na uwezo ndani ya bandari hiyo ambao hawana uwezo wa kuzalisha kwa manufaa ya kampuni.

Alisema ripoti ya uchunguzi dhidi  mwenendo wa bandari hiyo iliyofanywa na wataalam imekamilika na imebaini madudu mengi.

Waziri alisema ataikabidhi ripoti hiyo kwa bodi hiyo  iweze kuwawajibisha wahusika wote kwa kuwahamisha vituo vya kazi.

“Ripoti ninayo tayari na nitaikabidhi kwa bodi na kuna vigogo watatu waliosimamishwa wametajwa kwenye ripoti hiyo na wanahangaika kurejea kazini, hivyo naagiza bodi hakikisheni watu hawa hawarejei  kwa sababu  wanatumia hata fedha kujaribu kurejea.

“Inasikitisha sana kwa kuwa hata mimi nimefuatwa zaidi ya mara mbili na watu hawa ili wanilaghai lakini sitaki kuonana nao kwa kuwa watu hawa ni wala rushwa.

“Hawa  ndiyo walioisababishia serikali ipoteze mapato kutokana na mifumo mibovu waliyoitengeneza, kinachowasukuma warejee ni nini hapa jamani?”alisema Mbarawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles