28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

Aurier atakiwa Lille

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1), Lille, wanaitaka saini ya beki wa Tottenham na timu ya taifa ya Ivory Coast, Serge Aurier.

Habari hiyo inakuja kipindi ambacho Tottenham haionekani kumuhitaji Aurier, kama ilivyo kwa Moussa Sissoko anayeweza kutimkia Watford.

Kwa Aurier mwenye umri wa miaka 28, ni wazi kabisa kuwa hatahitaji muda mrefu kuzoea mikikimikiki ya Ligue 1 kwani alishawahi kucheza akiwa na Lens, Toulouse na PSG.

Nyota huyo amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na atavutiwa na ofa ya Lille kwa kuwa timu hiyo itashiriki Ligi ya Mabingwa msimu huu.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles