32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

AUAWA KWA DENI LA SH 5,000

Na AMON MTEGA-SONGEA


MKAZI wa Kijiji cha Litapatile, Kata ya Mtyangimbole, mkoani Ruvuma, Ndiko Bruno (24), ameuawa na mdeni wake kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kutokana na deni la Sh 5,000.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Gemini Mushy, alisema tukio hilo lilitokea Septemba 25, mwaka huu katika Kijiji cha Litapatile.

Akielezea chanzo cha tukio hilo, Kamanda Mushy alisema marehemu Bruno alikuwa akidaiwa Sh 5,000 na Januari Kayombo (26), mkazi wa kijiji hicho, ambaye aliamua kujichukulia sheria mkononi na kumchoma na kitu chenye ncha kali kifuani na kumsababishia umauti.

Alisema kutokana na tukio hilo, mtuhumiwa tayari amekamatwa na polisi kwa mahojiano na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili.

Kamanda huyo aliwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake, wafuate taratibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles