22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Akamatwa na SMG mbili, risasi 10

Kamishina Simon SirroAsifiwe George na Rehema Abdallah (A3), Dar es Salaam

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linamshikilia Shabani Ramadhani (35) mkazi wa Mbagala Mbande kwa tuhuma za kukutwa na bunduki mbili aina ya Sub Machine Gun (SMG) na risasi 10.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Aprili 12, mwaka huu wakati wa operesheni ya kuwatafuta wahalifu wa matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Alisema mtuhumiwa huyo, baada ya kukamatwa na SMG yenye namba UB-9686-1998 ikiwa na magazine ambayo haikuwa na risasi, alipohojiwa  aliwapeleka askari katika chumba cha Fatuma Salehe (20) ambaye ni mke wake mdogo, ambako walipopekua walikuta bunduki iliyokatwa kitako.

Kamanda Sirro alisema upelelezi unaendelea ili kubaini mmiliki wa silaha hizo, na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Katika hatua nyingine, jeshi hilo limesitisha operesheni ya kuwaondoa ombaomba katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kutokana na kile kilichoelezwa kuwa kazi hiyo inapaswa kuzingatia haki za binadamu.

Kamanda Sirro alisema ombaomba wote watakaoondolewa, lazima waandaliwe sehemu ya kukaa pamoja, chakula na kupewa nauli ili warudi makwao.

“Tumesitisha operesheni hii kwa muda ili kuweka mambo sawa, hawa ndugu zetu hawa hawakamatwi kama majambazi, wanatakiwa kupata chakula na gharama za kuwasafirisha,” alisema.

Kamanda Sirro pia alitoa onyo kwa kuwataka watu wanaochimba visima vya maji na kuviacha vikiwa havijafunikwa kuacha mara moja kwa sababu watoto wanaweza kutumbukia na kupoteza maisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles