22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Polepole alamba u-DC

Hamphrey PolepoleNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais Dk. John Pombe Magufuli, amefanya uteuzi wa wakuu wa wilaya wawili.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, ilisema Rais Magufuli amemteua Ally Salum Hapi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Hapi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Paul Makonda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Pia Rais amemteua Hamphrey Polepole kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma mkoani Mara, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (mstaafu) Zelothe Steven ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

Taarifa hiyo, ilisema uteuzi wa wakuu hao wa wilaya umeanza jana.

Kabla ya uteuzi huo, Polepole alikuwa mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Warioba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles