22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Ajali yaua 18 Mkuranga

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

WATU 18 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana katika Kijiji cha Kilimahwewa Kaskazini Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Ajali hiyo ilihusisha basi dogo la abiria (Coaster) lililokuwa likitoka Kijiji cha Magawa wilayani Mkuranga kwenda jijini Dar es Salaam ambalo liligongana uso kwa uso na lori la mizigo (Scania) lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Kusini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga, alisema ajali hiyo iliyotokea jana asubuhi ilisababisha vifo vya watu 18 na majeruhi 15 ambao walipelekwa katika Kituo cha Afya cha Kilimahewa.

Katika salamu zake za rambirambi, Rais Dk. John Magufuli, alivitaka vyombo vya usalama barabarani kuhakikisha vinachukua hatua madhubuti za kuzuia ajali za barabarani.

Aliwataka madereva na wote wanaotumia barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali ambazo zinagharimu maisha ya watu na uharibifu wa mali.

Rais Magufuli alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, kufikisha salamu zake za pole kwa familia za marehemu na kwamba anaungana nao katika kipindi hiki cha majonzi ya kuondokewa na wapendwa wao.

“Nawaombea familia za marehemu wote, ndugu, jamaa na marafiki kuwa na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, kuwapoteza Watanzania wenzetu kwa idadi kubwa namna hii, inaumiza sana,” alisema Rais Magufuli.

Mmoja wa wafiwa, Athumani Mtulya, alisema katika ajali hiyo alipoteza ndugu zake wanne.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles