24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Makonda: Usisafiri kwenda mikoani kama hauna sababu maalumu

Anna Potinus, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa wito kwa wakazi wa jiji hilo kupunguza safari za kwenda mikoani ikiwa hawana sababu maalumu za kufanya hivyo ili kuepusha kusambaza maambukizi ya ugonjwa wa homa ya mapafu unayosababishwa na virusi vya corona.

Makonda ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Aprili 16, wakati akipokea shehena ya vifaa vya kujikinga na virusi vya corona kutoka kwa Mfanyabiashara Maarufu Rostam Aziz ikiwamo barakoa, vitakasa mikono na mashine maalumu za kujitakasa kwa ajili kujikinga dhidi ya virusi hivyo.

Amesema hivi sasa hali imebadilika hivyo hakuna haja ya kwenda kusalimiana hovyo badala yake kila mtu akae nyumbani kwake ili kuepuka kusambaza au kupata maambukizi.

“Ninawapongeza sana wale wanaokataa wageni nyumbani kwao, jamani hali imebadilika sana kama wewe wa Dar es Salaam hauna sababu ya msingi kwenda mikoani baki hapa hapa tupambane na hili janga ili msije mkaenda kuwapelekea wengine maambukizi.

“Maambukizi ya mkoa wetu hayafurahishi sana idadi sio nzuri, ni vyema kwa kipindi hiki tukajilinda na kuwalinda tuwapendao pia kama hauna sababu ya msingi usiende mjini baki nyumbani kwako tunataka wanaoenda mjini wawe wana kazi ya kufanya huko,” amesema Makonda.

Aidha ametoa wito kwa wenyeviti wa mitaa kuzuia watu kukaa vijiwe ili kuepusha milundikano isiyo ya lazima na hivyo kuaagiza kuwachukulia hatua wale watakaokaidi maagizo hayo.

“Shule zimefungwa ili watoto wabaki nyumbani haina sababu ya kuruhusu watu walundikane wakipiga stori bila sababu ya muhimu mkiona hivyo mchukue hatua, tumieni nafasi zenu vizuri,” amesema Makonda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles