Na VERONICA ROMWALD-DAR ES SALAAM |
MKAZI wa Kigamboni mwenye umri wa zaidi ya miaka 60, jinsi ya kike (jina linahifadhiwa) amekutwa na ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa, kwa utaalamu unaitwa ‘congenital heart disease’.
Mama huyo alibainika wakati wa uchunguzi wa afya ya moyo uliofanyika juzi katika Hospitali ya Vijibweni, Kigamboni wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani.
Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Anna Nkinda alisema madaktari wameeleza mama huyo ana bahati kubwa kuendelea kuishi.
“Kulingana na madaktari watoto wengi wanaozaliwa na magonjwa ya moyo (congenital heart disease) hufariki dunia mapema, lakini mama huyu amebahatika kuishi hadi kufikia umri wa miaka zaidi ya 60,” alisema.
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.