LONDON, UINGEREZA
UMMA wa Waingereza umezidi kuwa na wasiwasi wa afya ya Malkia Elizabeth II baada ya mtawala huyo wa Uingereza kutohudhuria ibada ya mwaka Mpya kwa mara ya kwanza kipindi cha miongo kadhaa.
Aidha hakuweza kushiriki ibada ya Krismasi kama ilivyo kawaida kutokana na ugonjwa wa mafua.
Mtawala huyo aliyefikisha umri wa miaka 90Â Aprili mwaka jana, ameshiriki ibada zote za Krismasi katika Kanisa la Mtakatifu Mary Magdalene huiko Sandringham kila mwaka tangu familia ilipoanza kusherehekea sikukuu hiyo kanisani hapo mwaka 1988.
Hakuna kumbukumbu lini malkia huyo alikosa ibada ya Krismasi tangu atawazwe umalkia Februari 6, 1952, wakati alipokuwa na umri wa miaka 25.
Licha ya hali hiyo hakuna dalili zozote za kuashiria kuwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 90 ana matatizo makubwa ya kiafya.
Hata hivyp, kuugua mafua kwa muda mrefu kwa watu wenye umri mkubwa ni suaa lenye kuleta wasiwasi.
Mama yake mzazi alifariki dunia 2002 kutoana na matatizo yanayohusiana na mafua akiwa na umri wa miaka 101.