27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 16, 2024

Contact us: [email protected]

KAMPUNI YA APPLE YATISHIA KUIHAMA MAREKANI KUPINGA SERA ZA TRUMP

Donald Trump
Donald Trump

WASHINGTON, MAREKANI

KAMPUNI ya simu na tableti za Apple, inafikiria kuhamisha utengenezaji wa bidhaa zake nje ya Marekani kutokana na sera kali za Rais mteule Donald Trump ambaye ameapa kuhakikisha kampuni za nchini humo zinazalisha bidhaa ndani  ya taifa.

Na kama haitahama basi italazimika kuongeza bei ya bidhaa zake hatua itakayofanya bidhaa zake kuwa ghali zaidi  huku tayari zikiwa ghali.

Asilimia 90 ya bidhaa za Apple hutengenezwa China, Mongolia, Taiwan na Korea Kusini, hivyo kwa sera ya Trump itaiwia vigumu Apple kuendelea na shughuli zake kitu kilichoifanya kufikiria kuhamisha makao yake sehemu nyingine.

Kwa Apple, changamoto ni uwepo wa makao yake makuu Marekani, ni uwepo wa ofisi zake kuu ambako hutoa uongozi na ubunifu wa mawazo na mauzo ya bidhaa zake ambazo utengenezaji wake hufanyiwa nje ya nchi kupitia kampuni tofauti.

Ingawa Apple wanawazia kutengeneza  bidhaa zao nchini Marekani yaliko makao yao makuu, jambo hilo linaonekana kuwa gumu sana kwa sababu gharama za uendeshaji nchini humo ni kubwa sana ikilinganishwa na mataifa ya nje inakozitengenezea.

Kwa maana hiyo, kama ikitokea wafanyie yote Marekani basi hatua hiyo linamaanisha itakula wastani wa faida wanayopata kutokana na mauzo ya simu hiyo hatua inayoweza kuwafanya kuongeza bei ya bidhaa zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles