24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

ACT-WAZALENDO YAIBANA SERIKALI

NA LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM


CHAMA cha ACT – Wazalendo kimeitaka Serikali kufanya uhakiki wa vyeti kwa viongozi wote wa siasa na isipofanya hivyo kitafikisha suala hilo mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho, Ado Shaibu, alisema endapo Serikali haitawahakiki viongozi hao na mamlaka zinazohusika kutowachukulia hatua kwa kughushi vyeti, kitafungua mashtaka mahakamani.

“Malalamiko ya wananchi kuwa kuna viongozi  wamatumia vyeti feki na wengine wakituhumiwa kuwa na shahada batili ni ya muda mrefu.

“Ikumbukwe kiongozi ni kama dereva kwa hiyo kuwaacha kwa kisingizio cha kujua kusoma na kuandika ni sawa na kuwa na dereva ‘kihiyo’ anayeendesha gari lililo na abiria waelewa,” alisema Shaibu.

Alisema kitendo cha kutowahakiki viongozi hao kinapotosha mantiki nzima ya mchakato wa uhakiki na kuweka upendeleo wa dhahiri baina ya watumishi wa umma.

“Msingi wa mchakato huu ni kuhakikisha taifa linabaki na watumishi wenye sifa.

“Waziri Kairuki hakutaka kujiuliza iwapo viongozi wa siasa watathibitika kughushi vyeti ambalo ni kosa la jinai, haitawaondolea sifa yao ya uongozi,”alisema.

Kauli hiyo imetolewa ikiwa ni siku chache tangu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, kueleza kuwa uhakiki huo haukuwahusisha viongozi wa siasa kwa kile alichodai kuwa Katiba inawataka kujua kusoma na kuandika tu.

Waziri Kairuki alitoa kauli hiyo Aprili  28 mwaka huu, wakati akikabidhi taarifa ya uhakiki wa vyeti kwa Rais Dk. John Magufuli ambako   watumishi 9932 walibainika kuwa wanatumia vyeti vya udanganyifu na kutakiwa kujiondoa wenyewe kazini.

Alisema watakaokaidi watafikiswa katika vyombo vya dola.

Shaibu alisema uamuzi wa kutowahakiki viongozi wa siasa ni ushahidi wa dhahiri wa jinsi Serikali inavyohaha kuwalinda baadhi ya wateule na wanasiasa ambao wametuhumiwa na umma kwa makosa ya kughushi vyeti.

Alisema kitendo cha Rais kutangaza kuwasamehe watumishi wenye vyeti feki watakaojiondosha kazini wenyewe ni kinyume cha sheria na Katiba ya nchi kwa sababu hana mamlaka ya kufanya hivyo katia katiba.

 Alisema kwa mujibu wa sheria Rais hana mamlaka ya kumsamehe mtu anayetuhumiwa kufanya kosa la jinai iwapo mtu huyo hajafikishwa kwenye vyombo vya sheria na kuhukumiwa.

Mamlaka pekee aliyonayo Rais ni kutoa msamaha kwa wafungwa wanaotumikia kifungo, alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles