25.3 C
Dar es Salaam
Monday, January 17, 2022

ULIMWENGU ATAKA VYOMBO VYA DOLA VIDHIBITIWE

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam


MWANDISHI wa habari nguli nchini, Jenerali Ulimwengu, ameitaka Serikali kuvizuia vyombo vyake vya dola kuwashambulia waandishi wa habari.

Ulimwengu alisema hayo juzi usiku alipozungumza kwenye hafla ya utoaji tuzo za umahiri wa uandishi wa habari zilizotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).

“Ni nadra kumkuta mwanahabari akiwa amebeba kamera nzito halafu afanye fujo, sijawahi kuona labda ashushe kwanza kamera, afanye fujo, kisha arudi kuibeba aondoke zake.

“Si kweli kwamba wanaanzisha fujo wao (wanahabari) wanafanya kazi yao, mara nyingi wanapigwa kwa sababu polisi hawataki kile kinachorekodiwa kionekane katika jamii,” alisema.

Alisema iwapo kuna makatazo ambayo yanaelezeka au yanapaswa kuelezwa ni vema waambiwe namna ya kufanya kazi na si kuwapiga.

“Mara nyingi kama kuna kesi naona wanatengewa chumba na kutakiwa kukaa humo, kwamba wasitoke labda mtu aamue atoke mwenyewe litakalomkuta ni yeye, au labda asukumwe tu na wanahabari wenzake lakini si polisi,” alisema na kuongeza:

“Vyombo vya usalama vifunzwe vema majukumu yao jinsi ya kutambua mipaka yao, kuheshimu haki za binadamu na waandishi wafahamishwe juu ya mipaka halali iliyopo na jinsi watakavyoweza kutimiza majukumu yao bila kubughudhiwa wala kuumizwa”.

Ulimwengu alisisitiza kampeni za kupinga mateso, unyanyasaji na kuumizwa kwa waandishi wa habari nchini ziendelee kufanyika.

“Wanahabari waweke kumbukumbu sahihi na kamili za wana usalama waliowashambulia, wahakiki kiwango cha madhara waliyoyapata na inapofaa wawashtaki waliowaumiza na wawadai fedha nyingi kama fidia.

Aliwataka wanahabari kujenga mshikamano zaidi katika kutekeleza majukumu yao kwa jamii.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,717FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles