26 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Simba yamtambulisha beki kisiki wa Kenya ikiimarisha ulinzi

WINFRIDA MTOI, DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba, imewatambulisha rasmi wachezaji wake wawili wapya, aliyekuwa beki kisiki wa Gor Mahia na timu ya Taifa ya Kenya, Joash Onyango na mshambuliaji Charles Ilamfya kutoka timu ya Manispaa ya Kinondoni(KMC).

Wachezaji hao wawili walitambulishwa jana, siku ambayo klabu hiyo, pia ilikuwa inazindua nembo na jezi mpya, ambazo itazitumi a kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ilamfya ametua Msimbazi ili kuongeza uimara katika safu ya ushambuliaji ya Simba, ambayo pia ina wakali wengine akiwamoJohn Bocco na mfungaji bora wa msimu uliopita Meddie Kagere. Kagere alimaliza msimu uliopita wa Ligi Kuu akifunga mabao 22.

Kwa upande wa Onyango ambaye ni beki wa kati usajili wake una lengo la kuisuka upya idara wa ulinzi ya Wekundu hao hususani mabeki wa kati.

Msimu uliopita, Simba ilikuwa ikiwatumia Pascal Wawa, Erasto Nyoni na Kennedy Juma.

Wawa alijihakikishia namba lakini Nyoni na Juma walikuwa wakipishana.

Wapenzi wengi wa klabu hiyo walikuwa na imani ndogo na safu yao ya ulinzi  kutokana na Nyoni na Wawa kuonekana umri kuwatupa mkono na kutaka maingizo mapya.


Kwa mujibu wa Simba, usajili wa Ilanfya ni utekelezaji wa mapendekezo ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji Sven Vandenbloeck, ambaye alivutiwa na uwezo wake baada ya kumshuhudia akiwa na KMC.

“Kocha wetu aliuambia uongozi msajilini huyu kijana, miguu yake itatupa kitu kizuri Msimbazi, ni tumaini la baadae katika soka la nchi hii hususani upande wa washambuliaji,” ilisema taarifa ya Simba.

Kuhusu Onyango ni mwendelezo wa maboresho ya kikosi hicho kuelekea katika michuano ya kimataifa, ambapo Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tumeweka malengo makubwa msimu huu ya kufika mbali katika Ligi ya Mabingwa Afrika na mashindano ya nyumbani hivyo lazima pia klabu isajili mabeki na wachezaji wenye uzoefu mkubwa katika mechi kubwa kubwa, beki wa kimataifa Onyango ni mmoja wao,”ilieleza taarifa ya Simba.

Wakati huo huo, mchezaji mpya wa Wanamsimbazi hao Bernard Morrison jana alipamba uzinduzi wa jezi mpya ya timu hiyo, huku akiahidi kufanya mabukwa akiwa na kikosi hicho.

Morrison alisema amejipanga kuitendea haki jezi hiyo akianzia katika mechi ya kilele cha tamasha la Simba, Simba Day ambalo litafanyika Agosti 22,  mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles