25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

ACT, Chadema tutasimamisha mgombea urais mmoja – ZITTO

YOHANA PAUL Na SHEILA KATIKULA-MWANZA

KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, chama chake pamoja na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) vitaungana ili kusimamisha mgombea mmoja wa kiti cha urais.

Hayo aliyasema juzi jijini Mwanza wakati akizungumuza na waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano mkuu wa wajumbe wa chama hicho Jimbo la Nyamagana wakupata mgombea ubunge kwa jimbo hilo.

Zitto alisema vyama vya upinzani vyenye nia ya dhati kushirikiana kwa sasa ni viwili, hivyo anawahakikishia Watanzania vitasimamisha mgombea mmoja wa urais ambapo mchakato wa kisheria unafanyiaka  ili kufikia maafikiano.

“Hadi sasa sisi tunajua kitu gani kinachoendelea, tumejipanga ninachotaka kuwakikishia tu ni kwamba tutakuwa na mgombea mmoja wa upinzani.

“Mazungumuzo bado yanaendelea, yapo vizuri na dhamira yetu ni hiyo, hatuwezi kuwavunja moyo Watanzania, wanataka mabadiliko, na wanataka vyama vishirikiane nasi tutashirIkiana na hiyo ndiyo kauli ambayo naomba muwafahamishe wananchi,” alisema Zitto.

Kuhusu minong’ono ya kutoelewana kwa baadhi ya vyama vya upinzani, Zitto alisema hiyo inatokana na utofauti wa maono, sera na mikakati na hivyo kutokuelewana wakati mwingine ni jambo la kawaida.

 Alisema kuelekea Uchaguzi Mkuu chama chake kitakuwa tayari kushirikiana na vyama vyenye sera makini tu na si vinginevyo.

Kuhusu mfumo wa kamati kuu ya chama hicho kupitisha majina wa wagombea baada ya kura za wajumbe, Zitto alisema mfumo huo ni wa kurithi kutoka kwenye katiba ingawa ni lazima ifikie hatua vyama vya siasa viheshimu maamuzi ya wanaopiga kura ngazi ya chini.

Alisema hoja ya chama chake kuheshimu maamuzi ya wajumbe ni nzuri lakini kwa sasa ni vigumu kuitekeleza kwa sasababu ndani ya katiba ya vyama vyote maelekezo ni kwamba kamati kuu ndiyo inatakiwa kufanya maaamuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles