Mwandishi Wetu
KAMATI ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Mwenyekiti wake imewasilisha malalamiko katika Kamati ya Maadili dhidi ya wanafamilia watatu wa mpira wa miguu kwa kuchochea hisia za jamii, na kutoa vitisho kuhusu shauri lililokuwa mbele yake.
Taarifa iliyotolewa leo Agosti 14, 2020 na Ofiosa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo imwataja wanafamilia hao kuwa ni Mjumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, Zakaria Hans Poppe, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Simba, Haji Manara, na mchezaji Bernard Morrison.
Pia Sekretarieti ya TFF imempeleka Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli katika Kamati ya Maadili kwa kutoa taarifa ya uongo.
Wahusika watapewa malalamiko dhidi yao kwa njia ya maandishi pamoja na mwito wa kuhudhuria kikao cha Kamati ya Maadili.