Yvette aibuka na ‘Thankful’

0
290

KENTUCKY, MAREKANI


KUTOKA Kentucky nchini Marekani, mrembo anayefanya vizuri kwenye muziki wa ‘gospo’, ameibuka kivingine na wimbo, Thankful aliouachia hivi karibuni mtandaoni.


Akizungumza na MTANZANIA, Yvette mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, alisema wimbo huo umebeba ujumbe wa kumshukuru Mungu.


“Nimeachia video ya wimbo wangu mpya unaitwa Thankful katika chaneli ya YouTube, naamini nina mashabiki huko Afrika Mashariki hivyo naomba sapoti yao, naamini wimbo huu utawabariki watu wote,” alisema Yvette.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here