26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

JPM afanya mapinduzi mikataba ya madini

Na Mwandishi Wetu

HATUA ya Kampuni kubwa ya uchimbaji madini duniani ya Barrick Gold Corporation yenye makao makuu yake Canada, kuridhia kwa asilimia 100 kutekeleza makubaliano yote mapya ya kimkataba kati yake na serikali ya Tanzania, inatajwa na magwiji wa uchumi kuwa ya kimapinduzi na ya kwanza ya aina yake kupata kufikiwa sehemu yoyote duniani.

Barrick na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli wamekuwa katika mazungumzo juu ya namna bora zaidi na yenye manufaa kwa pande zote mbili ya uendeshaji wa migodi yake hapa nchini ambayo hitimisho lake limefikiwa kwa mafanikio wiki iliyopita.

Makubaliano ya kihistoria yaliyofikiwa Februari mwaka huu ambayo hatimaye yameridhiwa na Barrick pamoja na mambo mengine, yanaitaka kampuni hiyo na serikali ambao ni wabia kugawana kwa uwiano sawa wa asilimia 50/50 faida itakayopatikana katika uchimbaji wa madini.

Sambamba na hilo, pande hizo mbili zimefikia makubaliano ya kuifanya serikali ya Tanzania kuwa mwanahisa katika uchimbaji wa madini kwa kuwa na asilimia 16 ya hisa tofauti na ilivyokuwa awali.

Makubaliano hayo ambayo yanaweza yakawa chachu ya …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles