Shule ya Kilimani yatakiwa kuendeleza ushirikiano na wazazi

0
886

KOKU DAVID-DAR ES SALAAM

Uongozi wa Shule ya msingi Kilimani iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam umetakiwa kuendeleza bidii, maarifa, maadili na ushirikiano na wazazi  ili kuweza kuwasaidia watoto kufanikiwa kimaisha katika siku za usoni.

Hayo yalizungumzwa jana na Afisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Manispaa ya Kinondoni, Said Hanga wakati alipohudhuria sherehe ya maadhimisho ya miaka 10 ya shule hiyo sambamba na kuwaaga wanafunzi waliomaliza darasa la saba.

Alisema ushirikiano wa walimu  na wazazi utawezesha shule kufanya vizuri lakini pia watoto kuwa na nidhamu na maadili ambavyo wanafunzi wanatakiwa kuviendeleza katika maisha mapya ya elimu ya sekondari wanayoenda kuianza.

Naye mwalimu msaidizi wa taaluma wa Kilimani Ibrahim Azizi alisema kuwa msingi wa shule hiyo ni kuzingatia mambo ya msingi yanayohusu maadili katika makuzi yao ikiwa ni pamoja na maendeleo ya kitaaluma.

Alisema maendeleo ya taaluma yanaangalia nafasi ya watoto kuimarika katika ujuzi wa kujisomea na kuwa na ubunifu katika masuala ya taaluma ikiwa ni pamoja na uwezo wa kupambanua mambo tofauti yanayohusiana na utandawazi na changamoto katika maisha yanayomzunguka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here