Na DERICK MILTON
-BARIADI
HATIMAYE zaidi ya wananchi 1,000 wa Kata ya Lamadi, Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, jana walipiga kura ya siri kuwataja watuhumiwa wa mauaji ya watoto wilayani humo.
Hatua ilianza saa 5:02 asubuhi na kumalizika saa 7:34 mchana, ambako mamia ya wanawake wakiwa na watoto, wanaume na vijana walijitokeza kwa wingi kupiga kura.
Upigaji kura huo ulisimamiwa na maofisa wa Usalama wa Taifa kutoka za Wilaya za Itilima, Meatu na Maswa, huku mshangao mkubwa ukiwa ni kutokuwapo polisi.
Hata hivyo, Licha ya kukosekana polisi hatua hiyo ilienda salama hadi kukamilika, huku wananchi, mmoja baada ya mwingine wakipiga kura na kurejea sehemu waliokuwa wamekaa.
Mtanzania ilipata taarifa kutoka chanzo kimoja (hakikutaka kutajwa jina) kuwa kukosekana kwa polisi kulitokana na wananchi kulituhumu jeshi hilo wakati wa mkutano wao na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, Februari 11.
Kwenye mkutano huo wananchi walitaka ipigwe kura baada ya kueleza kutokuwa na imani na polisi wakidai askari hao wamekuwa wakiwakamata watu wanaotuhumiwa kwa mauaji hayo na baadaye kuwaachia.
Wakizungumza baada ya kupiga kura baadhi ya wananchi walisema wahusika watajulikana tu.
Walimshukuru RC Mtaka kwa kuwakubalia ombi hilo ambalo walieleza ndiyo njia pekee ya kukomesha matukio hayo.
“Tunakupongeza Mkuu wa Mkoa, umeonyesha uongozi wako, umeonyesha kuwatumikia wananchi, hakika tuna kiongozi bora.
“Hii kura ambayo tumepiga hapa inaenda kumaliza tatizo hilo, hofu hapa kwetu imekuwa kubwa,” alisema Alfred Nanai na kuongeza:
“Hili eneo ni maarufu hapa Lamadi, matukio yote ya uhalifu na ambayo ni mabaya kwenye jamii yetu yamekuwa yakimalizikia hapa, leo nina miaka 74 hapa ndiyo suluhisho la unyama huu”.
Hata hivyo wananchi hao walimuomba Mtaka kuwaruhusu …
Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.