Elizabeth Joachim Dar es salaam
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewapandisha kizimbani watu wawili akiwamo aliyekua Mkuu wa Manunuzi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula(NFRA),Mohammed Ally na kuwasomewa mashtaka mawili ya uhujumu uchumi na kusababisha hasara ya Sh Milioni 977.
Katika kesi hiyo, mshtakiwa mwingine ni Mkaguzi Mkuu wa Ubora wa Bidhaa za Ngozi wa Shirika la Viwango Tanzania(TBS), Peter Tarimo.
Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, leo Ijumaa Novemba, 9 Augustina Mbando,mawakili wa serikali Aneth Mavika na Fatma Waziri, walidai kuwa washtakiwa hao walitenda makosa kati ya Julai 16 na 30 mwaka 2013.
Amedai kwa makusudi, wakiwa wajumbe wa uthamini wa zabuni Namba AE-054/2013/2014/HQ/9/02 lot namba 01, walitumia madaraka yao vibaya kwa kumpendekeza na kumzawadia Kampuni ya Bajuta International T. Limited ili kushinda zabuni hiyo huku wakijua kuwa kampuni hiyo haikua na sifa.
Amedai katika zabuni hiyo, kampuni hiyo iliwasilisha nyaraka ambayo haikuendana na masharti yaliyoanishwa kwenye zabuni, jambo ambalo ni kinyume na sheria za manunuzi.
Amedai shtaka lingine linalowakabili washtakiwa hao ni pamoja na kushindwa kutimiza majukumu yao na kuisabaishia hasara NFRA ya Sh Milioni 977.
Wakili Mavika alidai kuwa, upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kuiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Wakili Mavika pia aliiomba mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa kwa mshtakiwa wa pili,Edward Mtango ili aweze kuunganishwa kwenye kesi hiyo.
Hata hivyo, Hakimu Mbando alikubaliana na ombi hilo na kutoa amri ya kukamatwa kwa mshtakiwa huyo huku akitoa masharti ya dhamana kwa washtakiwa Mohammed na Peter ya kuwataka kila mmoja kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja atasaini bondi ya Sh Milioni 165.
Hakimu Mbando pia aliwataka washtakiwa hao kuwasilisha hati zao kusafiria mahakamani hapo.
Hata hivyo,mshtakiwa wa kwanza, Mohamed alikidhi masharti ya dhamana huku mshtakiwa wa tatu,Peter akishindwa kukidhi masharti hayo na kupelekwa rumande na kesi hiyo kuahirishwa hadI Novemba 22 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa
[17:06, 11/9/2018] lulu ringo: http://mtanzania.co.tz/first-class-kuzindua-albam-mpya/