Mwandishi Wetu, Dodoma
Serikali imesema itawachukulia hatua watendaji wote waliosababisha kusambazwa kwa vitabu vya kiada vya darasa la nne vyenye makosa ya kimaudhui.
“Vitabu vya kiada vya darasa la kwanza hadi la nne vinaendelea kuzalishwa na kusambazwa kwa shule zote kwa masomo, zoezi limeanza kwa mikoa 12 na litakamilika Mei 30 mwaka huu.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha Aidha, amesema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia katika bajeti ya wizara hiyo.
“Zoezi la uhariri na uchapishaji limefanyika kwa umakini na vile vyenye makosa nipo tayari kukaa nao wabunge waliobaini makosa hayo ili kuangalia ni vitabu gani na kama yapo waliosababisha watachukuliwa hatua,” amesema.
Aidha, amesema rasimu ya muswada wa sheria ya bodi ya kitalaamu ya walimu unatarajiwa kuletwa bungeni mwaka huu kwani sasa upo unahakikiwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali.